May 8, 2017Wachezaji wa Ndanda FC wametishia kugoma kwenda mjini Mbeya kuichezea timu hiyo kwa kuwa hawana fedha, maji na chakula.

Wachezaji hao wamedai wanataka kugoma kwa kuwa hawajalipwa mshahara kwa miezi mitatu,.

Mbali na hivyo wamessema hawatasafiri kwenda kucheza mechi dhidi ya Prisons ya Mbeya kwa kuwa hata chakula wamekuwa wakila mara moja kwa siku.

“Tunakula mara moja kwa siku, hatuna chakula kitu cha kuziachia familia zetu. Hali yetu ni mbaya sana na kweli hatutaweza kupambana,” alisema Jackson Chove, kipa mkongwe wa timu hiyo.


Ndanda FC ni kati ya timu zinazopambana kuepuka kuteremka daraja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV