May 26, 2017






Mbao FC imekuwa kati ya timu zilizokutana na rungu la adhabu baada ya Kamati ya Saa 72 imekaa kupitia mambo mbalimbali baada ya Ligi Kuu Bara, kwisha.


Mechi namba 230 (Kagera Sugar 2 Vs Mbao FC 0).

Klabu ya Mbao imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na timu yake kutoingia vyumbani wakati wa mechi hiyo iliyochezwa Mei 13, 2017 katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Adhabu hiyo ni uzingativu wa Kanuni ya 14(48) ya Ligi Kuu.

Kesho Mbao FC itashuka dimbani kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kuivaa Simba katika mechi ya Kombe la Shirikisho la Azam.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic