May 2, 2017




Hatimaye fainali ya Kombe la Shirikisho kati ya Mbao FC dhidi ya Simba itafanyika Mei 28 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Msemaji wa TFF, Alfred Lucas amethibitisha kwamba uwanja utakuwa ni Jamhuri.

"Kweli ni Jamhuri, awali ilikuwa ni droo lakini sasa moja kwa moja tumetangaza Jamhuri," alisema leo.

Awali, kupitia mitandao ya kijamii, Rais wa TFF, Jamal Malinzi alitangaza uwanja utakaochezewa mechi utapatikana kupitia droo.


Malinzi alisema droo itafanyika ndani ya siku chache zijazo jambo ambalo lilizua mjadala mkubwa kati yake na mashabiki ambao walioenkana kumshangaza.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic