May 15, 2017




Uongozi wa Yanga unatarajia kumuweka kitimoto mshambuliaji wake, Donald Ngoma raia wa Zimbabwe kumjadili kutokana na vitendo anavyovifanya ndani ya timu hiyo ikiwemo ya kuondoka na kugomea kuichezea timu hiyo kwa kisingizio cha kuwa majeruhi.

Ngoma aliyetua Yanga misimu miwili nyuma, kwa msimu huu amekuwa na msaada kidogo ndani ya timu hiyo kutokana na kutocheza mara kwa mara kwa sababu ya majeraha ya goti ambalo limemfanya akose michezo mingi ya timu hiyo.

Katibu wa timu hiyo, Boniface Mkwasa, alisema wataongea kwa kina na mshambuliaji huyo juu ya safari yake ya Afrika Kusini alipoenda kutibiwa ambapo alizidisha siku ambazo alipewa ruksa ya kukaa huko.

“Tunatarajia kuwa na kikao na Ngoma kutokana na mwenendo wake kwa msimu huu ambapo amekuwa akikaidi baadhi ya vitu ambavyo tunakubaliana ikiwemo juu ya safari yake ya Afrika Kusini aliyoenda hivi karibuni.

“Tulimpa ruhusa ya kwenda kutibiwa huko ili akamalize tatizo lake la goti ambalo linamsumbua lakini yeye alipitisha siku ambazo tulimpa ruhusa na kuendelea kukaa huko bila ya idhini yetu na bila ya kuuambia uongozi lolote lile.

“Sasa tunataka tumbane kwa ajili ya kujua nini kilichotokea maana ilisemekana kuwa alifanya mazungumzo na baadhi ya timu hivyo tunataka kujua kama ni kweli au la,” alisema Mkwasa.

 SOURCE: CHAMPIONI



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic