May 17, 2017


Baraza la Wazee la Simba, limeibuka na kusema mabadiliko ya katiba yanafanyika kihuni.

Simba ilikuwa katika mchakato wa kubadili baadhi ya vipengele vya katiba ili iweze kuuza hisa zake na tayari Mfanyabiashara na mwanachama wa Simba, Mohamed Dewji "Mo" alishajitokeza kununua hisa asilimia 51 akiwekeza Sh bilioni 20.

Wazee hao wametaka mchakato kwa hatua sahihi ufuatwe badala ya uharakishaji wa mambo kama ambavyo inataka kufanyika sasa na wamemuandikia barua Rais John Pombe Magufuli.

Mratibu wa Baraza la Wazee la Simba, Felix Mapua amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwamba wameamua kumuandikia barua Rais Magufuli, wakiomba kumuona.

“Tunaona mambo yanapelekwa haraka na kihuni, tumeamua kumuandikia barua Rais Magufuli kupitia kwa Waziri wa michezo, Dk Mwakyembe.
“Tunaomba kumuona Rais Magufuli, tunaona hata iwe kwa dharura. Hata kidogo hatukubaliani na mambo yanavyokwenda na hatufurahi hata kidogo.

“Simba ni kubwa sana, kubwa kuliko hata Mohamed Dewji. Hivyo hatuwezi kukubali mambo yaende namna hii,” alisema.
1 COMMENTS:

  1. Hakuna lolote hao wazee wakae chini waangalie mpira unavyoendeshwa..Wao sio wa kumdis Mo leo baada ya kupata sponsor.. Ivi wakipewa simba ya sasa wanaweza kusajili na kulipa mishahara au wanaongea tuu..nimewasikiliza jana nkaona hawa wazee hawajui wanachokiongea na huu sio wa kipindi kile wachezaji wanacheza hata bila mshahara kwa mapenzi ya timu..sasa ni pesa tuu... kama wanadhani simba inaweza kuendeshwa kwa story za vijiwe vya kwahawa waache hizo ndoto za mchana..

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV