June 15, 2017Yanga imemalizana na mshambuliaji Ibrahim Ajibu Migomba.

Ajibu amejiunga Yanga kwa mkataba wa miaka miwili.

Taarifa kutoka Yanga zinaeleza Ajibu amemalizana na Yanga mchana huu baada ya kuwa wamefanya mazungumzo mfululizo tokea juzi.

"Tulikuwa hatujamalizana katika masuala fulani ya fedha, lakini sasa naona mambo yamekaa vizuri kabisa," kilieleza chanzo.

"Ukisema Ajibu ni mchezaji wa Yanga tayari, wala hautakosea," chanzo kilisisitiza.

1 COMMENTS:

  1. Basi sawa, na huku Ngoma anaenda Simba, sasa tuone nani kalamba dume, Ajibu ni mchezaji mzuri akiwa na mpira na si mgiganaji, yeye ni yule wa akupe umpe afunge au agige krosi, shida yake hakabi wala timu ikiwa imezidiwa hana faida, unamuona mtu kama Omog na Kocha wa timu ya taifa hamtumii sanaa kwani kama unataka kucheza game la kushambulia sana na kupata mabao ya haraka usimuweke Ajib.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV