Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema Juma Nyosso awatawasaidia kuimarisha safu ya ulinzi.
Maxime amesema Nyosso ni kati ya mabeki bora na ana imani naye.
“Mimi sipendi maneno, subiri ligi ianze utaona. Ninaamini atakuwa msaada,” alisema na hata alipoulizwa tena, akasema.
“Nyosso ninampokea na nina imani naye. Ndiyo maana nasema subiri ligi ianze.”
Kagera Sugar imemtwaa Nyosso ambaye mkataba wake na Mbeya City imemaliza akiwa kifungoni.
Nyosso alipatikana na hatia ya kumpapasa makalio nahodha wa Azam FC, John Bocco wakati huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment