June 11, 2017Kikosi cha Gor Mahia ya Kenya, kimeandika historia ya kuwa timu ya kwanza kubeba ubingwa wa SportPesa Super Cup.

Gor wamewatwanga wapinzani wao wakubwa AFC Leopards kwa mabao 3-0 katika mechi hiyo ya fainali iliyomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Fainali hiyo ilipewa jina la “Derby ya Mashemeji” ambayo ni kawaida kila timu hizo zinapokutana.

Kwa ushindi huo, Gor Mahia ndiyo watakaocheza mechi ya kirafiki dhidi ya Everton Julai 13 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Gor walionekana kuwa bora zaidi katika kila idara na hasa katika upangaji mashambulizi na umaliziaji.

Leopards inayonolewa na Mtanzania, Denis Kitambi ilishindwa kutoa makucha yake.


Kwani pamoja na Gor kuwa na mabao mawili, lakini ilionekana kushambulia zaidi hadi ilipopata bao la tatu katika dakika za nyongeza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV