June 11, 2017Kipa Aishi Manula, amemalizana na Simba kwa kusaini mkataba wa miaka miwili.

Taarifa zinaeleza, Simba wamemalizana na Manula mara tu baada ya kambi ya timu ya taifa iliyocheza jana dhidi ya Lesotho.

“Kweli amesaini miaka miwili, Simba inaendelea na kazi yake. Tafadhari waambieni wanachama na mashabiki watuamini, tunajitahidi kufanya kazi yetu,” kilieleza chanzo.

Tayari Simba ilikuwa imezungumza na Manula, lakini akaondoka kusafiri na timu ya taifa iliyoweka kambi nchini Misri.


Manula anakuwa mchezaji wa pili baada ya John Bocco kumalizana mapemaa na Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV