Imani Madega amesema kurejesha kwake fomu ya kugombea Urais wa TFF inaonyesha yuko tayari.
Madega amekuwa kati ya watu wa kwanza kurejesha fomu kuwania nafasi ya urais.
Uchaguzi wa TFF umepangwa kufanyika Agosti 12 mjini Dodoma.
“Kila kitu kinakwenda vizuri, nimerudisha fomu na hii inaonyesha kweli niko makini kuhusiana na hili. Sitazungumza sana hadi wakati wa kampeni,” alisema.
Madega atachuana na Jamal Malinzi anayeshikilia kiti hicho, Athumani Nyamlani, Shija Richard pia Wallace Karia.
0 COMMENTS:
Post a Comment