June 15, 2017



Nahodha wa Simba, Jonas Mkude atabaki Simba kwa asilimia 90.

Taarifa za ndani ya Simba zimeeleza Mkude anatarajia kuongeza mkataba na Simba ndani ya siku mbili.

Mkude ataongeza mkataba baada ya mazungumzo na viongozi wake kukamilika na imeelezwa kila kitu kiko vizuri.

Mmoja wa viongozi amesema: “Sisi na Mkude, tuko vizuri na huenda akasaini ndani ya siku mbili.”
Alipotafutwa Mkude amesema yuko katika mazungumzo yamefikia pazuri.

“Tusubiri kwanza ili kujua tumefikia wapi. Lakini mimi na viongozi tunajua tumefikia wapi,” alisema.

Tayari Ibrahim Ajibu ameamua kujiunga Yanga huku kukiwa na taarifa Abdi Banda na Mkude nao wamekuwa wakiwaniwa.


“Suala la kuondoka nalijua mimi. Lakini sasa bado niko Simba na ninaendelea na mazungumzo, tuliachie hapo kwanza,” alisisitiza Mkude.a

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic