June 16, 2017

 Timu anayoitumikia Mtanzania, Emily Mgeta ya Neckarsulmer imebeba ubingwa wa FA Kwa eneo lao nchini Ujerumani.

Kombe Hilo ni maarufu kama Baden Wurttemberg na sasa wamefuzu kucheza Germany Cup.

Mgeta alijiunga na klabu hiyo akitokea Polisi Moro ambayo aliichezea nusu msimu.

Kabla alikuwa ni mchezaji katika kikosi cha vijana cha Simba kabla ya kupandishwa timu kubwa wakati wa Kocha Zdravko Logarusic.

Hata hivyo, hakupata nafasi ya kucheza kwa kuwa kocha huyo kutoka Croatia alivutiwa zaidi na wachezaji wazoefu.

Mgeta ambaye anatokea mkoani Mwanza amekuwa tegemeo katika kikosi cha  Neckarsulmer hasa nafasi ya beki wa kushoto.

Hivi karibuni, alikumbana na balaa la kuumia na kulazimika kukaa nje kwa muda mrefu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV