June 20, 2017


 Ofisa wa juu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shija Richard amerejesha fomu ya kuwania nafasi ya Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Akionekana ni mwenye furaha, Shija amerejesha fomu yake katika ofisi za TFF leo na yuko tayari kwa ajili ya uchaguzi huo utakaofanyika Agosti 12 mjini Dodoma.Shija ambaye ni Meneja ndani ya Mamlaka ya Mapato Tanzania, alichukua fomu hiyo jana Jumatatu katika ofisi za TFF Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, ingawa hakuzungumza lolote kwa maelezo kuwa muda wa kampeni bado. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV