June 11, 2017


Hoteli za sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam zimefaidika kutokana na fainali ya SportsPesa Super Cup inayopigwa leo kwenye Uwanja wa Uhuru.

Fainali hiyo inawakutanisha watani kutoka Kenya, Gor Mahia na AFC Leopards na tayari watu wameanza kusogea katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, kuishuhudia.


Taarifa zinaeleza mashabiki wengi kutoka nchini Kenya wakiwemo waandishi wa habari wako nchini kushuhudia “Derby ya Mashemeji”.

Imeelezwa sehemu nyingi za hoteli hasa zilizo maeneo ya Chang’ombe zimepata wateja ambao wanajiandaa kwa ajili ya mechi hiyo.

Hata kwa hapa nchini, inaonekana mashabiki wengi wa Yanga na Simba watajitokeza wakiwa hayari wamegawanyika.


Simba wameamua kuishangilia Leopards ambaye ni mnyama kama wao na Yanga wao wako upande wa Gor Mahia ambayo huvaa jezi za kijani kama zile za Jangwani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV