June 11, 2017


Staa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo imeelezwa amejaaliwa watoto wawili mapacha.

Taarifa zinaeleza pamoja na hivyo, Ronaldo ameendelea kufanya jambo hilo siri kama ilivyo kwa mtoto wake wa kwanza, Ronaldo Jr.

Runinga ya Ureno kupitia channel yake ya SIC, imesema watoto hao wawili, mmoja wa kiume na mwingine wa kike wamepewa majina ya Eva na Mateo.

Lakini mambo yameendelea kuwa siri na Ronaldo hajasema lolote.


Ronaldo hajawahi kumtaja mama wa mtoto wake wa kiume na sasa taarifa zinaendelea kusambaa naye akiendelea kuwa kimya.

Kwa sasa yuko na mpenzi wake ni mrembo wa Kihispania aitwaye Georgina Rodriguez ambaye hivi karibuni ilielezwa kuwa ni mjamzito.

Lakini runinga hiyo ya kwao Ureno, imeibua mambo mampya kabisa ambayo hayakuwa yamewahi kusikika.






0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic