July 27, 2017Mwanamasumbwi Floyd Mayweather ndiye bondia aliyeingiza fedha nyingi zaidi kupitia ngumi.

Imeelezwa utajiri wake kwa sasa unafikia pauni milioni 261 na kumfanya kuwa mwanamichezo mwenye fedha nyingi zaidi.

Lakini safari yake ya utajiri inaonyesha mafunzo kwa kuwa katika pambano lake la kwanza mwaka 1996, alilipwa pauni 1,921 wakati sasa analipwa mamilioni ya fedha katika kila pambano.

Hii inaonyesha baada ya malipo ya kwanza, Mayweather alitaka kufanya vizuri zaidi na zaidi ndiyo maana amecheza mapambano 49 bila ya kupoteza hata moja huku akiongeza thamani yake kwa kiasi kikubwa.

Sasa yuko katika hatua za mwisho kujiandaa na pambano lake la 50 baada ya kutangaza kurejea, hili atacheza dhidi ya Conor McGregor.


PAMBANO LA KWANZA, 1996: £1,921
PAMBANO LA KWANZA UBINGWA WA DUNIA, 2001: £115,000 
Dhidi ya Zab Judah, 2006: £3.8m
Dhidi ya Shane Mosley, 2010: £30.7m
Dhidi ya Manny Pacquiao 2015: £169m-176m


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV