July 27, 2017


Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, ACP Barnabas Mwakalukwa amefanya ziara katika ofisi za Global Publishers jijini Dar es Salaam.

Mwakalukwa ametembelea Global Publishers na kujifunza mambo mbalimbali ya uandaaji wa habari katika chuma hicho cha habari, moja ya vyumba vikubwa vya habari nchini Tanzania.


Akiwa katika ofisi hizo, ACP Mwakalukwa aliongozwa na Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally ambaye alimuonyesha mambo kadhaa.

ACP Mwakalukwa pamoja na kujifunza mambo kadhaa, alihoji mambo kadhaa na mwisho kueleza ziara yake ilikuwa ina lengo la kukuza uhusiano.


Pamoja na hivyo, alipata nafasi ya kufanya mahojiano na Global TV, runinga ya mtandaoni inayotamba kwa kiasi kikubwa wakati huu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV