July 21, 2017




Shirikisho la Soka Afrika (Caf) limetangaza kuifutia Zanzibar uanachama.


Kamati ya utendaji ya Caf imekutana jana  mjini Rabat, Morocco na kuamua mambo kadhaa likiwemo hilo la Zanzibar.


Rais wa Caf, Ahmad Ahman amesema Zanzibar ilipewa nafasi hiyo kimakosa.
Amesema si sahihi kwa nchi moja kuwa na wanachama wawili wa shirikisho hilo.
Zanzibar ilipewa uanachama wakati wa utawala wa Issa Hayatou ambaye alikuwa akiungwa mkono na TFF chini ya Jamal Malinzi.

Hata hivyo, Hayatou aliangushwa na Ahmad ambaye aliibuka ushindi katika uchaguzi wa Caf.
Hivi karibuni, Caf ilitangaza kuipa Zanzibar uanachama wa Caf lakini ulitakiwa kupitishwa na kamati ya utendaji.

Hata hivyo, Zanzibar kuwa sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imefanya kuvuliwa tena uanachama huo na kuendelea kubaki kama ilivyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic