July 21, 2017




Bondia Mmalawi, Israel Kamwamba ametamba atamharibu sura Francis Miyeyusho wa Tanzania ambaye naye amesema atamtwanga Mmalawi huyo na kubeba taji la Afrika Mashariki na Kati.

Mabondia hao wanapanda ulingoni keshokutwa Jumapili kwenye Ukumbi wa DarLive na pambano lao litarushwa mubasharaa na Global Tv Online.

"Nitampiga vibaya Francis, nataka kuwa bingwa na niko makini na hili,” alisema Kamwamba ambaye hajawahi kupigwa.

"Nataka mkanda, nataka kuweka heshima nyumbani. Huyu Mmalawi lazima akae," alijigamba Miyeyusho.

Pambano hilo litarushwa moja kwa moja na runinga maarufu ya mtandaoni ya Global Tv Online.


Watazamaji watatumia simu zao za mkononi au kompyuta kushuhudia pambano hilo wakiwa majumbani. Kikubwa watakachotakiwa ni ku-subscribe kupitia mtandao wa You Tube kwa kuandika globaltvonline, halafu wanafanya hivyo na kugonga alama ya kengere ili wapate taarifa mara tu baada ya pambano kuanza kupitia simu zao za mkononi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic