July 21, 2017

MABINGWA WATETEZI, CAMEROON.

Unaweza kusema Tanzania ishindwe yenyewe baada ya  Shirikisho la Soka Afrika (Caf), kuongeza timu nane.

BAdala ya timu 16, sasa michuano hiyo itakuwa na timu 24, maana yake timu zilizo katika nafasi ya pili katika makundi kuwania kufuzu zitapata nafasi ya kucheza.

Hii inaanza moja kwa moja katika michuano ya mwakani yaani 2019 itakayofanyika nchini Cameroon ambao ndiyo mabingwa watetezi wa michuano hiyo.

Hii ni nafasi ya Taifa Stars kuingia kwenye Afcon kwa mara nyingine tena tokea mwaka 1980.

Mara kadhaa, Taifa Stars imekuwa ikifanikiwa kushika nafasi ya pili na si ya kwanza.


Huenda kama juhudi zitafanyika, maana yake Taifa Stars ina nafasi kubwa ya kushiriki kama itajipanga sahihi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic