July 21, 2017




Mwandishi Wetu, 
MICHUANO ya International Champions Cup iliyoanza mwaka 2013, imezidi kujichukulia umaarufu kwa kiasi kikubwa hadi kuanza kufananishwa na ile ijulikanayo kama Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Michuano hiyo hufanyika wakati wa kipindi cha maandalizi ya misimu mipya ya ligi kuu mbalimbali zikiwemo maarufu duniani.

Mfano, Premier League ya England, La Liga ya Hispania, Serie A ya Italia, Bundesliga ya Ujerumani na Ligue 1 ya Ufaransa na hizi ndizo ligi kubwa tano duniani katika mchezo wa soka.

Timu kubwa au maarufu zaidi za ligi hizo hupata nafasi ya kushiriki michuano hiyo na inawezekana kupatikana kwa mabingwa watatu kwa mkupuo kulingana na maeneo ambako timu zimekutana.

Uhondo huu kwa wapenda soka nchini wanaupata kupitia king’amuzi cha StarTimes ambacho kimepata kibali cha kuonyesha michuano hiyo. Umaarufu wake unapanda kwa kuwa unazikutanisha timu vigogo barani Ulaya ambazo mara nyingi huchuana katika Ligi ya Mabingwa Ulaya tena katika hatua za juu, mfano robo, nusu fainali au fainali hasa.

Wengi wenye ving’amuzi vya StarTimes wameanza kufurahia huduma hiyo lakini wanalazimika kutolala mapema kwa kuwa kutokana na tofauti ya muda, mechi hizo zinaonekana “usiku mnene”.

Hata hivyo, mashabiki wengi wa soka wameendelea kuzisubiri ili kuzishuhudia na zaidi wakiwa na kiu ya kuona wachezaji wapya wa timu zao wako vipi, msaada wao ukoje na itakuwaje watakapoanza kushiriki ligi za nchi husika. 

Timu nyingi zinakutana katika kipindi zikiwa na wachezaji wapya ambao zimewasajili kutoka katika timu nyingine kwa ajili ya kujiimarisha.

Hivyo mashabiki wanaweza kuanza kujua mwelekeo wa kikosi chao kipya kabla ya ligi kuanza kupitia michuano ya ICC inayorushwa moja kwa moja hapa nyumbani na StarTimes.

Leo alfajiri, mambo yanakwenda safi kabisa na itakuwa mechi ya watani wa Jiji la Manchester, yaani Man United dhidi ya Man City ikiwa imehamishiwa nje ya England.
Wakati kukiwa na Man United dhidi ya Man City, usisahau inakuwa ni Jose Mourinho dhidi ya Pep Guardiola. Hakuna kulala.


Leo IJUMAA:
Man United Vs Man City Saa 10:30 Alfajiri (IMECHEZWA NA MAN UNITED KUSHINDA 2-0)

Kesho JUMAMOSI:
Bayern Vs AC Milan    Saa 6:35 Usiku

Keshokutwa:
Juventus Vs Barcelona   Saa 7:00 Usiku
PSG Vs Tottenham Saa 9:00 Usiku
Real Madrid Vs Man United Saa 6:05 Usiku

Julai 25
Chelsea VS Bayern Saa 8:35 Usiku

Julai 26

Tottenham Vs Roma Saa 9:00 Usiku

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic