July 21, 2017


Pamoja na mbwembwe za bondia, Region Championi kutoka DR Congo, Mtanzania Iddi Pialali ametamba atamtoa shoo.

Mabondia hao wawili watapanda ulingoni keshokutwa Jumapili kwenye Ukumbi wa DarLive kuwania taji la Afrika Mashariki na Kati.

Pialali amesema amejipanga vema kushinda mkataba huo.

“Mchezo wa ngumi ni mgumu, lakini nimejiandaa na ninataka kushinda kwa kumchapa huyu Mcongo,” alisema.

Pambano hilo litarushwa moja kwa moja na runinga maarufu ya mtandaoni ya Global Tv Online.


Watazamaji watatumia simu zao za mkononi au kompyuta kushuhudia pambano hilo wakiwa majumbani. Kikubwa watakachotakiwa ni ku-subscribe kupitia mtandao wa You Tube kwa kuandika globaltvonline, halafu wanafanya hivyo na kugonga alama ya kengere ili wapate taarifa mara tu baada ya pambano kuanza kupitia simu zao za mkononi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic