July 12, 2017


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan amewakaribisha wachezaji wa Everton FC nyumbani kwake.

Wachezaji hao wakiwa na Wayne Rooney walifika kwa muda mfupi kumsalimia mama Samia ambaye atakuwa mgeni rasmi katika mechi ya kesho.

Everton FC kutoka England iko nchini kuivaa Gor Mahia ya Kenya ambayo ndiyo mabingwa wa SportPesa Super Cup.


Mechi hiyo itapigwa kesho saa 11 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na mama Samia ndiye mgeni rasmi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV