July 17, 2017


Kikosi cha Arsenal kiko nchini China kikifanya maandalizi ya msimu mpya wa 2017-18.

Wachezaji wake pamoja na soka wameonyesha wanaweza mambo ya Kung Fu pale walipoalikwa katika shughuli mbalimbali za kijamii hasa kwa utamaduni wa Kichina jijini Shanghai.

Kwenye sherehe hizo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Yuanshen, Olivier Giroud, Laurent Koscielny na Mohamed Elneny walikuwa wa kwanza kufika na baadaye Mesut Ozil, Alexandre Lacazette na Alex Oxlade-Chamberlain wakaungana nao na kushiriki mambo mbalimbali kama kucheza Kung Fu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV