July 16, 2017                      Simba Sports Club
Dar es salaam, Tanzania
16/7/2017.

       TAARIFA KWA UMMA.
   __________ 


Timu ya Soka ya klabu ya Simba kesho alfajiri,inatarajia kwenda nchini Afrika kusini,kwa ajili ya kuweka kambi ya maandalizi ya msimu,unaotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao. 

Kambi hiyo ya siku Ishirini itahusisha wachezaji wote waliosajiliwa kwenye klabu,kwa msimu huu wa ligi. 

Kwa upande wa wachezaji waliopo kwenye Timu ya Taifa,wao wataungana na wenzao,mara baada ya mchezo wa marudiano baina Taifa Stars na Rwanda,utakaochezwa wiki ijayo kule Kigali. 

Ikiwa huko nchini Afrika kusini,kikosi hicho pia kitapata fursa ya kucheza michezo kadhaa ya kujipima nguvu,kabla ya mchezo wake wa tarehe nane mwezi ujao(SIMBA DAY),Mechi ambayo klabu huitumia kutambulisha wachezaji wake na jezi mpya ya msimu,mchezo huo utapigwa hapa jijini Dar es salaam,kwenye uwanja wa Taifa. 

Wakati huo huo klabu ya Simba inaungana na wanamichezo na watanzania wengine,kumpa pole Waziri wetu mwenye dhamana ya michezo nchini Dr Harrison Mwakyembe kwa kuondokewa na Mkewe bi Linnah Mwakyembe. 

Tunamuomba Waziri Mwakyembe awe na subira yeye na familia yake katika kipindi hiki kigumu,na klabu itashiriki shughuli zote za msiba wa mama yetu Linnah. 

IMETOLEWA NA 

IDARA YA HABARI NA MAWASILIANO 


SIMBA NGUVU MOJA

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV