July 6, 2017
KUANZIA mwezi ujao, wateja wa King’amuzi cha StarTimes watapata nafasi ya kutazama Ligi Kuu ya Ujerumani ‘Bundesliga’, Ligi ya Ufaransa bure kwa mwezi mmoja.
Pia mwakani watatazama fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Urusi.

Kwa mujibu wa taarifa ya StarTimes kampuni inayoongoza kwa huduma bora na nafuu za matangazo ya kidijitali, wateja wa king’amuzi hicho watapata nafasi ya kutazama ligi hizo kupitia dishi na antena ambavyo vinauzwa kwa bei nafuu wakati huu wa maonyesho ya biashara ya kimataifa maarufu kama Sabasaba.

“StarTimes inawapa wateja ving’amuzi vya bei rahisi vilivyounganishwa na kifurushi  cha bure kwa mwezi mmoja, ambavyo vinapatikana kwa shilingi 78,000  kwa dishi na 47,000 kwa antena.

“Pia wateja wataweza kununua televisheni ya kidigitali kwa bei nafuu na kwa punguzo la asilimia nane ambapo kutakuwa na TV za inchi 40, 32 na 24 ambazo zina king’amuzi ndani yake,” ilisema taarifa hiyo.

Mbali na hayo, katika banda la StarTimes kutakuwa na bidhaa nyingine kama simu za kisasa na projekta ambazo zinapatikana kwa bei nafuu ambayo kila Mtanzania anaweza kumudu.

Lengo la StarTimes kufanya hivyo ni kumuwezesha kila Mtanzania aweze kumudu gharama za matangazo na kufurahia  ulimwengu wa kidijitali.


StarTimes inazo tamthiliya, filamu za Kiafrika na Ulaya, Kichina, Kihindi, vipindi vya watoto na mambo mengine mengi ya kiburudani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV