July 10, 2017



Ni siku chache baada ya kuibuka kwa taarifa kuwa kiungo mshambuliaji wa Simba, Mohammed Ibrahim ‘Mo’, huenda akajiunga na Yanga, meneja wa mchezaji huyo, Jamal Kisongo, ameibuka na kulikemea vilivyo suala hilo.

Mo ambaye amejiunga na Simba msimu uliopita akitokea Mtibwa Sugar, inadaiwa kuwa mara kwa mara amekuwa akisumbuliwa na viongozi wa Yanga wakimrubuni akajiunge na timu hiyo kwa ajili ya kuziba nafasi iliyoachwa wazi wa Mnyarwanda, Haruna Niyonzima anayedaiwa kujiunga na Simba baada ya mkataba wake kumalizika.

Kisongo alisema kuwa timu yoyote inayomhitaji Mo kwa sasa, haiwezi kumpata kwa sababu bado ni mali ya Simba na yeye pamoja na mchezaji huyo wanaheshimu mkataba walioingia na klabu hiyo.

“Nichukue nafasi hii tu kuwaambia hao Yanga kuwa, Mo kwa sasa haiwezekani kumpata, labda wasubiri mwakani.

“Mo bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Simba, kwa hiyo hawezi kuondoka klabuni hapo lakini pia yeye na mimi hatuwezi kufanya chochote kile kwa sasa, kwa sababu tunauheshimu mkataba huo na hatutaki kujiingiza katika malumbano yasiyokuwa na tija.
“Kama kweli wana mkataba, wasubiri atakapomaliza mkataba wake, lakini siyo sasa,” alisisitiza Kisongo ambaye pia ni meneja wa mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta anayecheza soka la kulipwa nchini Ubelgiji katika Klabu ya KRC Genk.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic