July 5, 2017


Taifa Stars imeshindwa kutinga fainali ya Kombe la Cosafa baada ya kufungwa kwa mabao 4-2 na Zambia.

Stars ilianza kupata bao kupitia Erasto Nyoni lakini Zambia wakasawazisha na kuongeza na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-1.

Baada ya Nyoni kuumia na kutolewa, mabeki wa kati Salim Mponde na Abdi Banda wakaonekana kuyumba na kutoa nafasi Zambia kufunga mabao mawili ya haraka.

Kipindi cha pili, Zambia walipata mabao mawili ya haraka na kuwa 4-1 lakini Simon Msuva alifunga bao jingine na matokeo ya mwisho yakawa 4-2.


1 COMMENTS:

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV