August 24, 2017


Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub Cannavaro amesema, amefurahishwa na wachezaji wenzake namna walivyopambana katika mechi dhidi ya Simba, jana.

Yanga ilicheza na Simba na kulala kwa mikwaju ya penalti 5-4 na Simba kubeba Ngao ya Jamii.


Lakini Haroub maarufu kama Cannavaro amesema, amefurahishwa kuona Yanga wakionyesha kiwango bora kabisa.

“Kweli wenzangu wamejitahidi sana, wameonyesha kiwango cha juu kabisa. Sioni cha kulaumu au kulalamika,” alisema Cannavaro ambaye hakucheza mechi hiyo.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic