Kiungo wa Mohamed Ibrahim amesema aliitamani penalti ya mwisho amalize mchezo wa Ngao ya Jamii, lakini bahati mbaya akapewa Mohamed Hussein Zimbwe, maarufu kama Tshabalala.
“Alipopewa Tshabalala kwa kuwa namwamini, nikaona bahati haikuwa yangu. Nilitamani kumaliza mchezo mimi.
“Nikaona Tshabalala amepata bahati hiyo na ni mchezaji mwenzetu ataifanya hiyo kazi vizuri lakini bahati mbaya haikuwa hivyo,” alisema.
Zimbwe alipewa penalti ya mwisho ambayo kama angefunga Simba ingeshinda kwa penalti 5-4, lakini kipa Youthe wa Yanga akapangua.
Baada ya hapo timu zikaanza kupigiana tena penalti moja moja na Yanga walianza na Juma Mahadhi, akakosa na kufuatiwa na Mo Ibrahim ambaye akafunga na Simba kushinda tena kwa 5-4.
“Alipokosa Zimbwe, ikawa nafasi ambayo niliitaka. Nilitamani kumaliza mchezo na nafasi ikaja kwangu, nilijiamini na nilijua nitaitumia vizuri,” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment