August 2, 2017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
________________

Kikao cha kamati ya utendaji ya klabu ya Simba iliokutana hivi karibuni,imemteua Dr Cosmas Kapinga kuwa Meneja mpya wa Timu ya Simba

Dr kapinga anachukua nafasi ya Mussa Hassan Mgosi ambae amepangiwa majukumu mengine ndani ya klabu. 

Kapinga ataanza kazi yake mpya,mara baada ya kikosi cha Simba kurejea nchini kutoka Afrika kusini,ambapo kwa sasa kipo katika maandalizi ya mwanzo wa msimu. 

Kwa upande wa Mgosi,sasa atakuwa kocha msaidizi na Meneja wa Timu ya vijana,sambamba na Nico Nyagawa ambae nae atakuwa kocha msaidizi wa kikosi hicho,huku pia akiwa mratibu,Kikosi hicho cha vijana kitaendelea kuwa chini ya kocha mkuu Nico kiondo. 

Katikati ya mwezi huu Mussa Mgosi atafanya mafunzo ya ukocha leseni C,ambayo yatampa fursa ya kuongeza ujuzi kwenye majukumu mapya ya ualimu ndani ya timu yetu. 

Wakati huo huo,benchi la ufundi la Timu ya Simba,limeridhishwa na maandalizi yao huko Afrika kusini,huku pia likiridhishwa jinsi kikosi cha Simba kilivyocheza jana na Klabu ya Orlando Pirates. 

Ingawa tumepoteza mchezo wetu wa jana,lakini tumeshaanza kupata mwelekeo wa kikosi,na katika siku chache zijazo,teyari tutakuwa tushapata kikosi cha kwanza"alisema Mwalimu Omog. 

Hapo kesho Timu hiyo itashuka kwenye dimba la Sturrock Park liliopo ndani ya Chuo kikuu cha Wits kilichopo Braamfontein Jijini Johannesburg kucheza mechi ya mwisho ya maandalizi nchini humo,dhidi ya Bidvest. 

Timu hiyo ndio mabingwa wa soka nchini Afrika kusini kwa sasa. 

IMETOLEWA NA... 

HAJI MANARA

MKUU WA HABARI SIMBA SC


SIMBA NGUVU MOJA

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV