August 27, 2017



Kampuni ya mchezo wa kubahatisha ya SportPesa imeanza kutekeleza ahadi yake ya kuufanyia marekebisho ya sehemu ya kuchezea 'pitch' ya Uwanja wa Taifa.

SportPesa ambao ni wa Dhamini wa klabu za Simba,Yanga,Singida United na Everton ya England, wameamua kushiriki shughuli za mpira hapa nchini kwa kuanza kuufanyia ukarabati uwanja huo hasa sehemu ya kuchezea mpira.



Baada ya ukarabati huo, uwanja wa Taifa utakuwa na mwonekano mpya na ubora wa kimataifa katika sehemu ya kuchezea.


SportPesa walimwaga mamilioni kutengeneza uwanja huo kwa nyasi ambazo zilitakiwa kutumika kwa muda wakati wa ujio wa Everton FC inayoshiriki Ligi Kuu England ambayo ulikuwa mwaliko wa SportPesa.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic