August 3, 2017Simba imecheza mechi yake ya pili ya kirafiki dhidi ya Bidvest ya Afrika Kusini na kupata sare ya 1-1.
Mechi hiyo imepigwa leo asubuhi kwenye Uwanja wa Sturrock Park jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Simba ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika 33 kupitia beki wake mpya, Erasto Nyoni.
Bao hilo lilidumu hadi katika mwisho wa kipindi cha kwanza cha mchezo huo.
Bidvest walisawazisha katika kipindi cha pili katika dakika ya 70.

Hii ni mechi ya pili ya Simba nchini humo, walianza dhidi ya Orlando Pirates, mechi ambayo walilala kwa bao 1-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV