Azam FC imesema imemalizana na Kagera sugar katika lile saga la mshambulizi Mbaraka Yusuf na sasa yuko huru kuichezea.
Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi amesema wamemalizana na Kagera Sugar ambao wametoa barua maalum ya kumuachia Mbaraka aitumikie Azam FC.
"Jana tulifanya kikao na Kagera Sugar na mwisho tumefikia mwafaka kuhusiana na suala hili na sasa Mbaraka ni mchezaji halali wa Azam FC," alisema Jaffar.
Baada ya Azam FC kumsajili Mbaraka, Kagera Sugar ilifungua kesi ya madai TFF ikipinga Azam FC kumtumia Mbaraka kwa kuwa ni mchezaji wake halali.

0 COMMENTS:
Post a Comment