Sare ya bila kufungana kati ya Simba dhidi ya Mlandege kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, leo, imeanza kuzua mjadala.
Mashabiki wengi wa Simba wamekuwa wakichangia mitandaoni wakionekana kutofurahishwa na sare hiyo.
Mashabiki hao, wamekuwa wakilalama kuhusiana na safu yao ya ushambulizi wakiamini haijafanya kazi sahihi.
Presha inaonekana inaanza kupanda mapema huku mashabiki wakitaka safu hiyo kufanya kazi ya kufunga mabao.
Tokea katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar baada ya Simba kushinda kwa bao 1-0 ilionekana wazi mashabiki hao hawakufurahishwa na hali hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment