August 18, 2017




SIMBA SPORTS CLUB
DAR ES SALAAM
18-07-2017


            TAARIFA KWA UMMA
         _________

Klabu ya Simba kesho Jumamosi itaendelea na Semina elekezi kwa wanachama wa wilaya za Ubungo, Kinondoni , na Ilala , zenye lengo la kuwajengea uelewa mpana zaidi juu ya muundo mpya wa klabu, uliotokana na mabadiliko makubwa ya katiba yaliyofanywa na wanachama hao. 

Semina hiyo ya tarehe 19-8-2017, itaanza saa 6:00 mchana kwenye jengo la Ngawaiya liliopo Manzese Argentina upande wa kushoto kama unaelekea Ubungo,katika Barabara kuu ya Morogoro. 

Pia Siku ya Jumapili hii ya tarehe 20-8-2017,kuanzia Saa mbili asubuhi,klabu itafanya Mkutano mkuu maalum wenye lengo hilo,ili taratibu za kuingia kwenye muundo mpya zianze kufanya kazi. 

Mkutano huu muhimu na wa kihistoria, utafanyika pale pale tulipofanyia Mkutano mkuu wa kawaida wiki iliopita, Mwalimu Nyerere International Conference Centre uliopo maeneo ya Ocean road hapa jijini Dar es salaam. 

Tunawaomba wanasimba kokote walipo waje kuweka historia hii muhimu,historia itakayofanywa muandikwe kwa wino wa dhahabu, Historia ya kuitoa klabu ilipo na kuipeleka mbele zaid, kiuchumi, kibiashara, kimafanikio ya uwanjani, na pia kuwa klabu ya kwanza nchini kuingia katika muundo huu,unaokusudia kuifanya Simba iwe moja ya klabu bora kabisa Afrika. 

Mwisho

Niwaambie maandalizi ya Mkutano wa Jumapili ni kabambe na kila kitu kimekaa sawa, pengine kuliko Mkutano wa wiki iliopita. 


IMETOLEWA NA... 

HAJI S MANARA

MKUU WA HABARI SIMBA SC 


SIMBA NGUVU MOJA

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic