Kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa imezidi kuipa jeuri Everton baada ya kumwaga pauni million 45 kumnasa kiungo kutoka Swansea.
Gylfi Sigurdsson amemwaga wino kuichezea Everton kwa miaka mitano na atakuwa akipokea mshahara wa pauni 100,000 kila wiki.
.
Tayari kiungo huyo ametua Goodison Park na kuanza kazi chini ya Kocha Mholanzi, Ronald Koeman.
’SportPesa ambao ni wadhamini wa Simba, Yanga na Singida United haps nchini, ndiyo wadhamini wakuu wa Everton ambao tokea wamepata udhamini huo wameonekana kuwa wakali katika usajili.
0 COMMENTS:
Post a Comment