September 3, 2017



Kocha wa Yanga, George Lwandamina anatarajia kurejea nchini leo, tayari kuanza kazi.

Lwandamina alilazimika kusafiri kwenda kwao Zambia baada ya kupata msiba wa kufiwa na baba yake mzazi.

Lwandamina aliiambia SALEHJEMBE kwamba angerejea leo ili kuendelea na kazi.

Pamoja na msiba huo mkubwa kwake, Lwandamina aliamua kurejea haraka ili kupambana kuhakikisha kikosi chake kinafanya vizuri.

Kocha huyo mtaratibu anatarajia kurejea leo jioni na kesho ataendelea na kazi ya kukinoa kikosi chake.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic