September 3, 2017


Mwandishi mkongwe wa michezo nchini, Saleh Ally “Jembe”, ametua katika uwanja wa Old Trafford jijini Manchester.

Mwandishi huyo alipata mwaliko kutoka katika timu ya wakongwe ya Manchester United na ile ya Barcelona na kuwa mwakilishi wa Salehjembe na gazeti la Michezo la Championi.

Saleh Ally amepata nafasi ya kufanya mahojiano na zaidi ya wachezaji watano kutoka pande zote za Barcelona na Manchester United.

Lakini amepata nafasi ya kujifunza mambo mbalimbali ya biashara yanayohusiana na Manchester United.

Pamoja na hivyo, alipewa nafasi ya kutembea katikati ya uwanja huo, jambo ambalo ni aghalabu kwa mtu asiye mchezaji au kocha kuruhusia kukanyanga nyasi za uwanja huo.


Salehjembe aliruhusiwa kuingia katikati ya uwanja mara tu baada ya mechi na kujifunza mambo kadhaa kuhusiana na nyasi za uwanja huo ambao unaaminika ni bora zaidi duniani sawa na ule wa Emirates unaomilikiwa na Arsenal FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic