September 30, 2017



Klabu ya Simba wamefikia uamyzi mmoja tu kuhusiana na suala la kumuuza kiungo wake wa pembeni Shiza Kichuya, kwamba hawatafanya hivyo.

Simba wanaamini Kichuya ana yhamani kubwa lakini timu kutoka Uarabuni iliyokuwa inamtaka, inaonyesha kutaka kutoa fedha kidogo kwa sababu nyingiii ambazo wao wanaona hazina msingi.


Hivi karibuni, Simba inayoshika nafasi ya nne katika Ligi Kuu Bara, ilikuwa na mipango ya kumuuza Kichuya anayesifika kwa kuchonga kona maridadi zinazoingia zenyewe wavuni wakati mwingine.

Hata hivyo, mipango hiyo ya Simba imekufa baada ya klabu iliyokuwa ikimtaka Kichuya kutaja dau dogo la usajili na hata ilipotakiwa kuongeza ikagoma.

Bosi mmoja ndani ya Simba huku akitaka hifadhi ya jina lake, amesema wamesitisha mpango wa kumuuza
Kichuya kwani klabu iliyomtaka imewatajia dau dogo.

“Klabu iliyomtaka Kichuya imetutajia dau dogo na sisi tumeona haipo sawa na hivyo hatutamuuza tena labda itokee timu nyingine itakayokuwa na dau tunaloona linafaa kwa mchezaji wetu.

“Hatupo katika mipango ya kuzima ndoto za mchezaji lakini tunapaswa kuuza mchezaji kwa maslahi siyo kumuuza mchezaji kwa sifa tu, hiyo haipo sawa,” alisema bosi huyo mwenye nguvu ya ushawishi Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic