September 30, 2017



Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, kesho Jumapili inaingia kambini kujiandaa na michuano iliyokuwa mbele yao,
lakini imeomba mechi za kirafiki na Simba na Yanga.


Kikosi kitakachoingia kambini kitakuwa na vijana 50 ambao 23 kati yao ni wale waliokuwa Serengeti Boys walioshiriki Kombe la Mataifa Afrika kwa Vijana, Mei, mwaka huu huko Gabon.


Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Kocha Mkuu wa timu za vijana, Kim Poulsen, alisema kikosi hicho kitakaa kambini kwa muda wa wiki mbili na kucheza mechi mbili za kirafiki za ndani.

“Tunaingia kambini Jumapili, lakini tukiwa kambini kwa muda wa wiki mbili ningependa kikosi changu kicheze dhidi ya timu za vijana za Simba na Yanga kwani tumepanga kucheza mechi mbili za kirafiki.

“Naamini mechi hizo zitatuweka fiti kwa ajili ya mechi zetu
zinazofuata na naamini Simba na Yanga watakubali tucheze mechi hizi za kirafiki,” alisema Poulsen.


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic