September 5, 2017



Nimeona baadhi ya watu ambao naamini ni mashabiki wa soka na watakuwa si wa Simba kwa kuwa wanaonekana kutofurahishwa na Msemaji wa Simba, Haji Manara.

Inaonekana Manara amewakwaza kutokana na mazungumzo yake ya kujigamba anapozungumza jambo na hasa anapoizungumzia klabu yake au kuwagusa watani wake Yanga.

Post zinazotembea mitandaoni zinaonyesha moja kwa moja baadhi ya watu wakimshambulia Manara kupitia ulemavu wa ngozi.

Wote tunajua mwenzetu Manara ni mlemavu wa ngozi, jambo ambalo hakulitaka na wala si la kumuumiza kwa kuwa ni majaaliwa ya Mwenyezi Mungu.

Kinachonifurahishwa kwa Manara ni mtu a nayejikubali na amekuwa anaendelea na maisha yake vizuri tena akionyesha namna ambavyo mtu kama yeye anavyoweza kuishi vizuri na maisha ya kawaida kabisa.

Niseme navutiwa naye kwa namna anavyoishi bila ya kujali au kutaka kuonyesha ni mwenye hofu au asiyejiamini au mwenye upungufu.

Manara anaweza kuwa mfano kwa wengine ambao kama wana upungufu au ulemavu basi wakaingiwa hofu na kujiona wao ni wanyonge. Badala yake wajikubali na kufanya majukumu yao ya kila siku kama watu wengine.

Kinachonisikitisha ni kuona watu wakimsakama Manara hadi kufikia kuzungumzia suala la kutaka kuuza ngozi yake. Jambo ambalo ninaamini sote tunalipinga na wala haliwezi kuwa utani hata kidogo.

Anayesema vile anaweza kuwa amevuta bangi? Anaweza kuwa mwendawazimu? Au niamini moja kwa moja ni kichaa asiyejua kwamba ameehuka!.

Hili ni jambo linalosikitisha sana, nimemuonea Manara huruma lakini niendelee kumtia moyo kwamba hata kama ni shabiki wa Yanga ndiye kafanya hivyo, lakini Yanga ina watu wengi sana wanaojitambua na hawawezi wakawa wajinga namna hiyo isipokuwa majuha wachache kama hao walioandika.

Hasira za mpirani au utani wa mpirani hauwezi ukasababisha kumdhalilisha mwanamke, mwanaume au mtu mwingine yoyote. Si sahihi kumuonyesha Mwenyezi Mungu amekosea.

Lakini bado ninaona kama tunavyojua Serikali ina mkono mrefu, basi uwafikie hao wahusika waliofanya upuuzi huo ili siku nyingine iwe mfano kwa wengine waliozoea kufanya namna hiyo jambo ambalo ni baya kabisa na likiachiwa likaendelea basi tutatanua wigo wa dharau na dhariri, jambo ambalo mwisho linaweza kutuingiza matatizo kwa kuwa si wote wanaweza kuwa na uvumilivu kama alionao Manara.

Lakini bado ninaamini wanaotaka kumkosoa Mwenyezi Mungu kwa kazi yake kwa kuwa amewaumba wakiwa na kila wanachoona kiko sahihi, basi siku moja atawarejeshea laana ili wajue anafanyaje kazi.

Ushauri wangu, hata kama ni utani wa Yanga na Simba au utani wa kimpira, basi sote lazima tujue kuna mipaka ya mambo na hakuna ubishi, lazima tuheshimiane na kupendana.


10 COMMENTS:

  1. Ni kweli wanastahili kukamatwa kwa kosa la kutishia uhai..mm naona serikali ifanye kazi yake

    ReplyDelete
  2. Busara ndiyo msingi wa jambo lolote hapa duniani

    ReplyDelete
  3. Wahenga walinena ujafa hujaumbika; hawa wanaomziaki Manara, kama hawatapata watoto wenye ulemavu wa ngozi basi wasishangae wakikumbana na mwingine wa aina yoyote ile. Mungu pishia mbali.

    ReplyDelete
  4. matusi yake kwa tshishimbi ndio yanamponza na yeye heshimu uheshimiwe udhalilishaji anaomfanyia tshishimbi kama sio mtu wa mpira tena msemaji wa klabu ambae anajua fika kwamba neno lake ni kauli ya timu anaenda kupost utumbo kama ule hio laana yako ndugu haimpati yeyoteeeeee yule itampata kama angekua anaonewa ila ila anatoa matusi akirudishiwa matusimnatoa laana? ajifunze utani na udhalilishaji akiweza kuvitofautisha hivyo nadhani hata hawa wapuuzi wanaomdhihaki kwa ngozi yake watakua hawana cha kujitetea kwa MUNGU na kwentye sheria

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hakuna anayeona kama manara anakosea yote anayosema, kejeli,vijembe yote ni sawa sasa kwa kuwa ameingia kwenye vita asitegemee watu wachague silaha hivyo ni vyema wanaomtetea manara waanze kwanza kumshauri manara mwenyewe maana aongei kama mtu wa mpira kabisa...

      Delete
    2. MUNGU anaona vile ambavyo mnafikiri, Kilema akichekwi wala kudhiakiwa, bali Uchafu na vitu vingine anavyofanya makusudi binadamu vya kijinga na kwa makusudi, maumbile ya MUNGU hayachekwi, sote ss tunategemea kupata watoto kama sio ss bhas ndugu zetu

      Delete
    3. Kila kitu hutokea kwa Sababu,unapomzarau Tshishimbi umewazarau wanatanga wote yaliyomkuta yanatokana na yeye mwenyewe

      Delete
  5. Hao wanaomdhalilisha Manara nao si vilevile wanapata watoto. Ni lazima wafahamu aliewanyima wao ndie aliyempa Manara na kejeli kama hizo huenda zikawadhuru kizazi chao

    ReplyDelete
  6. Mbona yeye anavyodhalilisha wenzie hamlalamiki!Tofautisheni utani na udhalilishaji anao ufanya manara msipende kuangalia upande mmoja.Shida wewe saleh ni mmoja wa wadau wa simba unaona an avoid halo misha yanga unapata furaha.Ni ujinga kuwaza ukimuambia mtu kilema na wewe utazaa kilema huo ni upumbavu wa mawazo.Mwambieni abadilike awe professional aache umbumbu wa kashfa sababu yeye kilema basi watu wamuogope.

    ReplyDelete
  7. Ni vema kuwa na uchaguzi mzuri wa maneno.Manara ni binadamu Kama binadamu yeyote.Inabidi pia awe na staha wakati akizungumza na vyombo vya habari.Ni vema pia ashauriwe namna bora ya kutoa habari.Mambo mengi ameyasema hovyo lakini suala ya Tshishimbi kufananishwa na Shilole limemgharimu.Aheshimu watu na Kazi zao naye ataheshimika tu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic