September 3, 2017


Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Ally Samatta amesema kitendo cha yeye kutofunga bao katika mchezo dhidi ya Botswana siyo cha kushangaza kwa kuwa timu ina wachezaji 11 na kinachotakiw ani ushirikiano wa pamoja ndiyo maana ikaitwa timu.

Samatta alisema hayo baada ya mchezo wa kirafiki baina ya timu hizo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ambapo Taifa Stars ilishinda mabao 2-0 yote yakifungwa na Simon Msuva

Katika mchezo huo Samatta alionekana kutocheza katika kiwango chake kilichozoeleka na hivyo kuwapa hofu baadhi ya mashabiki waliohudhuria mchezo huo.

“Hii ndiyo maana ikaitwa timu, siyo lazima Samatta afunge, akifunga mwingine au mimi nikicheza chini ya kiwango huku timu ikipata ushindi yote ni sawa, siku hazifanani lakini kwa ufupi timu yetu ilikuwa na uwezo mzuri kuliko wao (Botswana),” alisema Samatta ambaye ni mshambuliaji wa Genk ya Ubelgiji.

Aliongeza kwa kusema: “Botswana walijitahidi ila ilikuwa lazima wafungwe maana hawana kikosi bora zaidi yetu. Tungeshangaa kama sisi tusingeshinda, maana hatuna sababu kwa sasa.”

Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga amesema amefurahishwa na wachezaji ambao amewaita kwa mara ya kwanza katika kikosi hicho na akiahidi kuzidi kuwapa nafasi wengine ambao hajawahi kuwaita.

Ushindi huo wa Taifa Stars ni sita kwa Mayanga toka akabidhiwe mikoba ya kukinoa kikosi hicho kutokea kwa Charles Boniface Mkwassa ambaye sasa ni Katibu Mkuu wa Yanga.

Lakini, Mayanga ameiongoza Taifa Stars kucheza mechi 12, ambazo sita akishinda, tano akitoka sare na kufungwa mechi moja.

Kocha Mkuu wa Botswana 'The Zebras', David Bright yeye alimsifu kipa Stars, Aishi Manula ambaye anaona amekuwa kizingiti kikubwa cha wao kukosa matokeo chanya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic