WIKIENDI hii ligi nyingi za soka duniani zimesimama kwa muda, kuna mikiki ya timu za taifa, moja kati ya ligi ambazo zimesimama kwa muda ni Ligi Kuu ya Ujerumani ‘Bundesliga’.
Bundesliga imesimama huku tayari timu zote zikiwa zimeshaingia viwanjani kucheza mechi mbili kila upande na moto ni kama umeshaanza kuwaka, kwani ushindani ni mkali na timu zinaonekana kuwa vizuri. Wababe wa ligi hiyo, Bayern Munich ambao ni mabingwa watetezi, wapo pointi sawa na timu nyingine tatu, wote wakiwa wameshinda michezo miwili huku vita ya kufunga nayo ikionekana kuanza kwa kasi.
Bundesliga itaendelea wikiendi ijayo lakini katika michezo iliyopita kwenye ligi hiyo ambayo inaonyeshwa mubashara na King’amuzi cha StarTimes, Bayern wakiwa ugenini walipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Werder Bremen ambao wameanza msimu vibaya kwa kupoteza michezo yote miwili. Vigogo wengine wa ligi hiyo, Borussia Dortmund walijibu mapigo kwani wakiwa nyumbani walipata ushindi wa pili mfululizo kwa kuifunga Hertha BSC mabao 2-0.
Wengine wenye pointi sita sawa na wababe hao wa juu ni Hannover 96 ambao nao wakiwa nyumbani walishinda bao 1-0 dhidi ya Schalke 04 huku Hamburger SV wakitangulia kuifunga Köln mabao 3-1. RB Leipzig ambao msimu uliopita walikuwa tishio kiasi cha kukwaruzana na Bayern kwenye mchakato wa kuwania ubingwa kabla ya kulegea dakika za mwisho, walianza ligi vibaya kwa kipigo lakini wikiendi iliyopita waliamka na kupata ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya Freiburg. Upande wa pili mchakato wa kuanza kupigania nafasi ya kuwa
kileleni kwenye ufungaji bora nao umeshaanza, kama ilivyokuwa msimu uliopita, straika Robert Lewandowski wa Bayern Munich ameshaanza kung’ara, mpaka sasa ameshafunga mabao matatu. Wakati yeye akiwa ameshacheka na nyavu mara tatu, mpinzani wake, Pierre-Emerick Aubameyang wa Borussia Dortmund ameshacheka na nyavu mara mbili. Kumbuka wawili hao ndiyo ambao walikuwa na ushindani mkali hata msimu uliopita ambapo Aubameyang alimaliza msimu akiwa mfungaji bora kwa kufunga mabao 31 huku Lewandowski akiwa amefunga mabao 30. Wikiendi ijayo mtifuano unaanza mapema siku ya Ijumaa ambapo Hamburger SV baada ya kuanza vizuri watakutana na wabishi RB Leipzig kwenye Uwanja wa Volkspark. Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu kwa kuwa Hamburger watakuwa wana nia ya kuendeleza msimu wao vizuri huku.
NA: SALEH ALLY
0 COMMENTS:
Post a Comment