September 11, 2017

INAWEZEKANA kwa sasa kocha Arsene Wenger anaonekana hafai kitu machoni pa watu wote, anatajwa kwamba mbinu zake zimekwisha, hana makali tena, amechoka, anazingua na amepewa majina mengi ya kumkashifu kutokana na mwenendo wa timu yake ya Arsenal hivi sasa. 


Lakini Mfaransa huyu ana rekodi ya aina yake. Taarifa ikufikie kuwa, Wenger ameshinda mechi nyingi zaidi za Ligi Kuu England akiwa na Arsenal, kuliko ukijumlisha mechi zote ambazo makocha wengine 19 wameshinda katikaklabu zao za sasa kwenye ligi hiyo. 

Yaani ukijumlisha mechi zote ambazo Jose Mourinho, Jurgen Klopp na wengine walizoshinda kwenye Premier wakiwa na klabu zao za sasa, wote hawafikii idadi ya mechi ambazo Wenger ameshinda akiwa na Arsenal. 

Wenger ameshinda mechi 458 katika mechi 793 ambazo ameiongoza Arsenal lakini makocha wengine wote 19 wameshinda jumla ya mechi 379 katika mechi 907, kabla ya mechi za wikiendi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic