September 11, 2017

AMA kweli hakuna ufalme unaodumu milele! Beki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’au Zimbwe Jr  alikuwa kama mfalme wa nafasi ya kushoto msimu uliopita pale Simba na aliweka rekodi ya kucheza mechi zote za ligi, lakini mambo yamebadilika msimu huu, amepata mpinzani na amepigwa benchi mechi mbili mfululizo kwenye ligi.

Juzi Simba ilicheza dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar na kutoka suluhu. Tshabalala alikuwa benchi.

Tshabalala hadi sasa ameshindwa kufua dafu mbele ya beki mpya wa timu hiyo, Erasto Nyoni ambaye amejiunga na klabu hiyo hivi karibuni akitokea Azam FC.

Kocha Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog amekuwa akimpatia Nyoni nafasi ya kucheza kila wakati kutokana na kuonyesha uwezo mkubwa tangu alipojiunga na timu hiyo.

Akimzungumzia mchezaji huyo, Omog alisema: “Nyoni ni mchezaji mwenye faida kubwa anapokuwa uwanjani, mbali ya kucheza nafasi ya beki wa kushoto lakini pia ana msaada mkubwa kwa mabeki wa kati na pindi tunapokuwa tunashambuliwa.

“Anajua kukaba vizuri lakini pia anajua kuanzisha mashambulizi, kwa hiyo ni mtu muhimu sana katika kikosi changu.

“Kuhusu Tshabalala ni mchezaji mzuri lakini siwezi kuwatumia wote kwa pamoja ila atacheza tu, mechi bado ni nyingi.”


CHANZO: CHAMPIONI

1 COMMENTS:

  1. acha unwfik tshabalala katoka majeruhi hayupo fit 100% sasa unataka acheze hivyo hivyo wkt wapo wachezaji wengine? ndyo maana ya kusajil kikosi kipana chenye wachezaji wazur

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic