October 13, 2017



Yanga imeonyesha kuwa inajua ugumu wa mchezo wao wa kesho dhidi ya Kagera Sugar.

Tayari kikosi cha Yanga kimetua mjini Bukoba kwa ajili ya mechi yao ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar.

Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema wanajua uwezo wa Kagera Sugar na si timu ya kubeza.

"Kweli tunawaheshimu Kagera kama timu inayoshiriki ligi kuu, lakini sisi tumejipanga kwa ajili ya kucheza na kushinda.

"Tunataka kushinda na kuchukua pointi zote tatu, hivyo tunajua itakuwa mechi ngumu lakini tutakachopambana na kushinda," alisema.

Cannavaro amesema kikosi chao kilichotua Kagera salama salimini, kipo katika kiwango kizuri na tayari kwa mechi hiyo ya kesho.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic