October 11, 2017




Kutokana na uwezo mkubwa ambao wamekuwa akiuonyesha, kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simon Msuva, kocha wa timu hiyo, Mzambia, George Lwandamina, amemwambia kama ataendelea kujituma zaidi, basi siku si nyingi atakwenda kucheza soka Ulaya.

Msuva ambaye kwa sasa anaitumikia Klabu ya Difaa Al Jadida ya Morocco aliyojiunga nayo msimu huu akitokea Yanga, katika michezo miwili ya kirafiki ya hivi karibuni akiwa na kikosi cha Taifa Stars dhidi ya Botswana na Malawi, amefanikiwa kufunga mabao matatu.



Msuva amesema Ijumaa iliyopita alikutana na Lwandamina kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar, ikiwa ni muda mfupi baada ya mazoezi ya Taifa Stars na kumwambia anavutiwa na kiwango chake anachokionyesha kila siku.

"Ijumaa baada ya kumalizika kwa mazoezi yetu ya Taifa Stars, nilipata fursa ya kukutana na kocha wangu wa zamani Lwandamina ambapo alinisifia sana huku akisema kuwa kiwango changu kwa sasa ni kizuri.

"Hivyo amenitaka niendelee kupambana tu kwani uchezaji wangu alivyouona amenitabiria siku si nyingi nitafika mbali sana kisoka kwani umri bado unaniruhusu na endapo nitakuwa fiti zaidi, basi hata Morocco sitakaa naweza kwenda Ulaya.

"Nilifurahi kumsikia akiniambia hivyo maana yeye pia ni mmoja wa walimu wazuri ambao wamechangia mimi kufikia mafaniko haya mpaka sasa nacheza Morocco, kwa muda mfupi alipokuja Yanga aliniamini na kunipa nafasi ambayo leo imenisaidia sana.


"Napata faraja sana ninapoona watu wataalamu kama yeye wanatambua ninachokifanya, namuomba Mungu aendelee kunijalia niweze kufika huko wengi wanakonitabiria maana ndoto yangu pia ni kufikia mafanikio ya kucheza Ulaya," alisema Msuva.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic