October 11, 2017



Beki Mtanzania anayeitumikia Baroka FC ya Afrika Kusini, Abdi Banda anaamini kiungo wa ulinzi wa Simba, Jonas Mkude ana nafasi ya kucheza soka nchini humo.

Banda ambaye sasa ameanza kuchipukia vizuri katika Ligi Kuu Afrika Kusini amesema nafasi ya Mkude kucheza soka na kufanya vizuri katika nchi ya Afrika Kusini ni kubwa.

Mkude ni kati ya wachezaji waliokwenda kwenye majaribio ya kucheza soka Sauzi na kufuzu katika klabu ya Bidvest kabla ya Simba kumzuia kutokana na dau dogo la usajili walilotangaziwa.

"Nikwambie mimi nina muda mchache tangu nimejiunga na Baroka, lakini nikuhakikishie ni tegemeo kwa hivi sasa katika timu yangu hii mpya mchezaji yeyote ambaye anajua ana uwezo wa kucheza na hapa nchini hana nafasi basi ajaribu kuja Sauzi.

"Na hiyo imetokana na kujiamini pale ninapopewa nafasi ya kucheza, kwani ninatimiza majukumu yangu vizuri ambayo ninapewa na kocha wangu kabla ya mechi.


"Hivyo, kwa hapa nchini wapo wachezaji wenye uwezo wa kucheza soka Sauzi, hivyo basi ikaja ikatokea mchezaji akapata nafasi ya kuja kucheza soka hapa nchini, basi kikubwa anachotakiwa ni kutimiza majukumu yake pekee na kujiamini,"alisema Banda ambaye ni rafiki mkubwa wa Mkude.

Kabla ya kwenda kucheza soka la kulipwa Sauzi alikuwa akiitumikia Simba na akajiunga na Baroka baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu uliopita wa ligi kuu.

Banda amesema wapo wachezaji wengi wenye uwezo wa kucheza soka la kulipwa hapa nchini lakini tatizo ni nafasi pekee.

Banda alisema, soka la Sauzi siyo gumu kiasi cha mchezaji mwingine kushindwa kucheza kutokana na viwango kutotofautiana sana na wachezaji hapa nchini.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic