October 11, 2017



Bosi wa benchi la ufundi la JKT Ruvu, Bakari Shime ‘Mchawi Mweusi’ baada ya kushinda mechi zote nne kwenye Ligi Daraja la Kwanza ameibuka na kusema anaona African Lyon inaweza kuvunja rekodi hiyo Ijumaa kwenye mchezo wao utakaochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru kutokana na uzoefu wa wapinzani wao.

Kwenye Kundi A walilomo, JKT Ruvu inaongoza kwa kuwa na pointi 12 huku African Lyon ikishika nafasi ya pili kwa pointi saba.

Shime amesema anawashukuru vijana wake kwa juhudi walizofanya kwa kushinda mechi zote nne lakini mchezo wao unaofuata dhidi ya African Lyon unaweza kufuta rekodi hiyo kwani wapinzani wao hao ni wazoefu.

“Kwanza niwashukuru vijana kwa kazi nzito waliyofanya ya kushinda michezo yote minne, lakini mchezo wetu dhidi ya African Lyon utakuwa mgumu kwani hawa wapinzani wetu ni wazoefu kwenye ligi hii kwani kabla ya kushuka daraja walikuwemo.
“Sisi ni wageni kwenye ligi hii lakini malengo yetu ni kupata ushindi hili kurudi kwenye ligi kuu,” alisema Shime.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic